Skip to main content

Featured

Who are thefundedtrader?

  In this blog post, we will be discussing TheFundedTrader, a popular prop firm that offers traders the opportunity to trade with significant capital and potentially earn a share of the profits without risking their own money. What is TheFundedTrader? TheFundedTrader is a prop trading firm that provides traders with a unique opportunity to trade with a funded account. The company was founded in 2016 and has quickly become one of the most popular prop trading firms in the industry. How does TheFundedTrader work? The process of becoming a funded trader with TheFundedTrader is straightforward. Traders must first pass a qualification process, which involves trading a simulated account and demonstrating consistent profitability. Once a trader has passed the qualification process, they are given a funded account to trade with. The funded account comes with a set of rules and parameters that the trader must follow. These rules are designed to manage risk and ensure that the trader is usin...

ZIJUE FAIDA ZA KUNYWA MAJI KWA WINGI

Maji ni muhimu sana kwa afya yako, ukinywa maji kwa siku katika kiwango kinachotakiwa kiafya utaondokana na matatizo mengi ambayo mengine ungelazimika kutumia dawa mfano vidonge vya kupunguza maumivu (pain killers) na matatizo mengine yanayohusiana na uchovu wa mwili.   

Kabla sijaorodhesha faida mbalimbali ni vizuri ujue, je kama ukipungukiwa na maji mwilini ni athari au mataizo gani unayopata? Ukipungukiwa na maji mwilini unaweza kujisikia uchovu, kichwa kuuma, ngozi kukakamaa kutokana na kukauka, chakula kutosagwa vizuri ambapo unaweza pata shida kujisaidia haja kubwa nakadhalika.


Vilevile kama ukipungukiwa na maji mwilini utaweza kuwa na hizi dalili,

  • Kuhisi kiu au wakati mwingine hata kwikwi.
  • Kuhisi njaa. (Watu wengi hudhani kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kula chakula, lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kunywa maji.)

Je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (ikiwa glasi 1 ina ujazo wa 250ml) sawa na lita 2 kwa siku.


Baada ya kujua dalili za ukosefu wa maji mwilini pamoja na matatizo utakayopata kama hutokunywa maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili. 


Hizi ni tabia nzuri za kiafya za kuzizingatia.
  • Kila uamkapo asubuhi kunywa angalau glasi moja (1) ya maji.
  • Kila unapotaka kula, kunywa maji kabla ya kuanza kula chakula chako. Vilevile kunywa maji wakati ukiendelea kula na mwisho wa kula chakula kunywa maji tena.
  • Kabla ya kuanza kufanya mazoezi pendelea kunywa maji kwanza. Kunywa maji glasi 1 au 2 dakika 30 kabla ya kuanza kufanya mazoezi.
Kwakuwa maji ni muhimu na yana kazi nyingi mwilini, zifuatazo ni faida za maji mwilini kiafya.

1. Maji huboresha ngozi.


Seli za ngozi zinahitaji maji kwaajili ya utendaji kazi mzuri wa kazi zake ikiwemo kulinda ngozi kwa kupambana na magonjwa mbalimbali yakiwemo eczema, psoriasis na hata makunyanzi na kukauka kwa ngozi. Hivyo ukitaka kuonekana mwenye ngozi nzuri kama ya mtoto penda kunywa maji kwa kiwango kinachotosha kila siku kuboresha afya ya ngozi yako.

2. Maji husaidia katika utendaji kazi wa ubongo.


Ukitaka kuwa mwenye akili safi na mwepesi wa kufikiri na kutatua mambo mbalimbali yanayohitaji kutumia akili, pendelea kunywa maji pamoja na vyakula vyenye kusaidia seli za ubongo kufanya kazi zake vizuri. Ubongo unahitaji maji, hewa safi ya oxygen na vyakula vyenye virutubisho kama njugu mawe, mafuta ya samaki (fish oil), nyanya na mbegu za maboga.



3. Maji husaidia usagaji wa chakula.


Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula (digestive system) hutegemea sana maji katika ulainishaji wa chakula na hivyo kuwezesha virutubisho vya chakula kutumika vizuri na mwili, kwakuwa maji hulainisha chakula, pia huepusha kupata choo kigumu (constipation).

4. Maji husaidia kuondosha sumu na taka mwilini.


Licha ya maji kuwa ni sehemu kubwa ya miili yetu pia ni kitu ambacho kinawezesha viungo vingine muhimu kama moyo katika usukumaji damu yenye kiwango kikubwa cha oxygen ambayo inabeba maligafi nyingi na kupeleka sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika ini na kwenye figo ambapo uchujaji wa taka mwilini hufanyika.

5. Maji husaidia kupunguza maumivu mbalimbali kama ya kichwa pamoja na mgongo.


Licha ya kuwa na sababu nyingi za mtu kupata maumivu ya kichwa lakini pia ukosefu wa maji mwilini ni sababu moja wapo ya kichwa kugonga kwasababu ya kupungukiwa na mahitaji muhimu kama oxygen ambayo husafirishwa na damu ambapo maji husaidia kurahisisha shughuli hizo.

6. Maji huusaidia mwili kupigana na magonjwa mengi kama ya mafua, tumbo, saratani za aina mbalimbali na matatizo mengine ya figo.


Maji pamoja na juisi ya malimao husaidia sana kupooza magonjwa kama ya kikohozi, mafua, kuchafuka kwa tumbo, satani ya tumbo na kibofu cha mkojo nakadhalika. Maji yanaweza kukuepusha au kupunguza makali ya magonjwa hayo kwa kusaidia mwili wako kuongeza kinga ya mwili.

7. Maji husaidia kupunguza uzito.


Kama nilivyosema hapo awali wakati mwingine unaweza hisi kuwa unahitaji kula kumbe unahitaji kunywa maji kwakuwa umepungukiwa na maji mwilini. Ni mara ngapi umekuwa ukitamani kula chakula kwa pupa lakini baada ya kunywa maji ukajikuta unakula kidogo kuliko ulivyotegemea hapo awali. 

Uzito wa mwili hutegemea sana ulaji wa chakula pasipo kufanya mazoezi, maji pia husaidia kuondoa taka za vyakula vya mafuta (fats by-products) na kukuwezesha uwe mwenye afya bora.

8. Maji husaidia kuboresha misuli na kulainisha jointi za viungo vya mwili.


Maji ni chanzo cha nguvu mwilini, misuli huifadhi nguvu ya ziada itakayotumika iwapo nguvu ya mwili itapungua. Kunywa maji kulingana na mahitaji ya mwili wako ili kuwezesha utumikaji mzuri wa chakula na uhifadhi wa uhakika wa nguvu mwilini. Maji pia yatakusaidia kulainisha viungo vyako vya mwili kama jointi za kwenye magoti, vidole vya mikono na miguu n.k.

Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na makala hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako! 

Comments

Popular Posts