Matumizi ya Asali ni mazuri kwa afya yako lakini ikiwa tu utatumia ASALI HALISI na sio asali ILIYOCHAKACHULIWA. Ukitumia asali halisi utapata matokeo unayoyategemea na sivinginevyo.
Kutambua asali halisi fata mtiririko huu:-
1.Chukua glass unayoweza ona ndani kwa urahisi.
2.Jaza maji angalau nusu
3.Dondoshea asali taratibu kwenye glass yenye maji kama inavyoonekana kwenye picha.
4.Asali halisi inatakiwa iende mpaka chini na kutulia na isijichanganye na maji.
Kama asali uliyonayo sio halisi pindi itakapogusa maji tu itajichanganya na maji hayo.
Alisema njia ya pili ni kuiweka Asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha ikiwa
njiti hiyo itawaka basi Asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka inakuwa ni feki.
Aidha, Kamote aliongeza kuwa wizara yake imekuwa ikiwasisitiza wafanyabiashara
wa bidhaa hiyo kuwa waaminifu na kuwauzia wateja waoe bidhaa halisi na wale ambao bidhaa zao zinagundulika zimechakachuliwa ziharibiwa.
Aliongeza kuwa njia nyingine ni kuonja bidhaa hiyo na kwamba iliyokachuliwa kwa
kuchemsha inatoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi.
TOFAUTI YA ASALI YA NYUKI WADOGO NA NYUKI WAKUBWA
Asali za NYUKI WAKUBWA na WADOGO zina tofautiana katika mambo kadhaa na hvyo ni muhimu kujua tofauti hizo kabla hujanunua ili kua na uhakika.
NYUKI WADOGO
1. Ni nyepesi zaidi kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24
2. Ina ladha ya UCHACHU ingawa ni tamu sana.
3. Mara nyingi ina rangi ya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoenda kwenye WEUSI
NYUKI WAKUBWA
1. Ni nzito kuliko ya nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 17 hadi 20.
2. Ni tamu moja kwa moja bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki wadogo
3. Ina rangi nyingi kuanzia NYEUPE, NYANO, KAHAWIA ILIYOPOA, KAHAWIA ILIYOKOZA n.k
Hizo ni tofauti za muhimu kuzijua kwani zitakuwezesha kupata asali unayoitaka na kuepuka kuibiwa.
NJIA RAHISI YA KUANGALIA UHALISIA WA ASALI
Unaweza tumia njia hii ukiwa mahali popote na kwa mda mfupi kabisa.
1. Chukua asali kiasi kidogo
2. Chukua mshumaa wako ulio vizuri
3. Dumbukiza pamba ya kwenye mshumaa kwenye asali kidogo na kisha tingisha mshumaa wako kuondoa asali ya ziada kwenye pamba.
4. Jaribu kuwasha pamba ya mshumaa wako
5. Pamba ya mshumaa ikiwaka moto na kutozima basi tambua asali hiyo ni HALISI na haijachanganywa na kitu kingine kama maji.
6. Mshumaa ukigoma kuwaka jua asali hiyo sio halisi kwani itakua imechanganywa na vitu vingine kama maji n.k
Comments
Post a Comment